Moto uliowaka kwa siku 52 wazimwa

0
279

Vikosi vya zimamoto nchini Canada vimefanikiwa kuzima moto wa msituni ambao umewaka wa siku 52 mfululizo katika jimbo la British Colombia na kusababisha madhara.

Zaidi ya hekari 83,000 za misitu zimeteketezwa na moto huo wa msituni na habari zinasema mabadiliko ya tabia nchi huenda yakawa ndio chanzo cha moto huo.

Wadau mbalimbali wa mazingira nchini Canada wanataka serikali ya nchi hiyo kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanyia marekebisho ya sera za tabia nchi nchini humo ili kuokoa mazingira.