Mkuu wa Majeshi wa Mali afukuzwa kazi

0
572

Rais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali amemfukuza kazi Mkuu wa Majeshi wa  nchi hiyo,  ikiwa ni siku moja tu baada ya kutokea kwa mauaji ya watu 134,  ambao ni wafugaji katika kijiji cha Fulani kilichopo kwenye mji wa Mopti.

Pamoja na kumfukuza kazi Mkuu huyo wa Majeshi, Rais Keita pia amepiga marufuku kikundi cha Wanamgambo wa Dan Na Ambassagou katika mji huo, kwa madai ya kuwa kiini cha mauaji hayo.

Mkuu huyo wa Majeshi wa Mali amefukuzwa kazi baada ya kuwepo kwa madai kuwa,  Jeshi la nchi hiyo limekua likiwapatia silaha Wawindaji wa jamii ya Dogon ili wawashambulie wafujaji hao wa kijiji cha Fulani.

Wakati wakitekeleza mauji hayo yanayoelezwa kuwa ni ya kikatili, Wawindaji hao wa jamii ya Dogon walikua wamevalia mavazi ya kijadi ya uwindaji na walikua wakitumia silaha mbalimbali ikiwa ni pamoja na bunduku , visu, mapanga, mishale na upinde.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa, baada ya wauaji hao kufika kijiji katika kijiji cha Fulani walichoma moto karibu nyumba zote za wafugaji  pamoja na mali zao.

Mapigano katika mji huo wa Mopti nchini Mali hasa kwenye kijiji cha  Fulani,  yamekua yakitokea mara kwa mara  ambapo wawindaji hao wa jamii ya Dogon na wafugaji wa jamii ya Fulani wamekua wakigombea ardhi na maji.