Mji wa Bambari wakombolewa

0
204

Vikosi vya Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), vimeukomboa mji wa Bambari baada ya kuwa chini Waasi toka siku ya Jumanne.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati imesema kuwa, askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na wale wa nchi hiyo kwa sasa ndio wanaoudhibiti mji huo, na tayari Waasi hao wamekimbilia msituni.

Taarifa zaidi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati zinaeleza kuwa, Wakazi wa mji wa Bambari walioukimbia mji huo kwa kuhofia mapigano wameanza kurejea katika maeneo yao.

Jamhuri ya Afrika ya Kati inatarajia kufanya uchaguzi Mkuu siku ya Jumapili.

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imekuwa ikimshutumu Rais wa zamani wa Jamhuri hiyo, – François Bozizé kwa kushirikiana na vikundi vyenye silaha ili kuiondoa serikali iliyopo madarakani, tuhuma ambazo amezikanusha.