Miss England kuwatibu waathirika wa Corona

0
1431


Miss England apumzisha taji lake na kurudi kazini kama daktari wakati wa janga la Corona
Mlimwende Bhasha Mukherjee anatarajia kurudi kazini kama daktari baada ya siku 14 za kujitenga kutokana na janga la Corona.


Mlimbwende wa urembo ambaye alipewa taji ya Miss England mwaka 2019 amerejea nchini Uingereza kutoka kazi ya kutoa misaada ya nje ya nchi ili kuendelea na kazi yake ya udaktari kutokana na janga la corona.


Bhasha Mukherjee alichukua mapumziko ya kazi kama daktari baada ya kushinda taji la urembo na kuwakilisha England katika mashindano ya dunia ya urembo.