Misri waendelea na maombolezo

0
460

Wananchi wa Misri wanaendelea na maombolezo ya siku tatu kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak, aliyefariki dunia jana Febrauri 25, 2020 akiwa na umri wa miaka 91.

Mubarak aliondoka madarakani mwaka 2011 kutokana na shinikizo la wananchi wakati wa vuguvugu la mapinduzi ya nchi za kiarabu, yaliyosababisha viongozi wengi kuondoka madarakani.

Mubarak ameiongoza Misri kwa muda wa miaka 30, jambo ambalo Wananchi walikuwa wakidai kuwa wamechoshwa na utawala wake.

Serikali ya Misri imetangaza kuwa mwanasiasa huyo ambaye pia awali aliwahi kupata kiharusi na kufunguliwa mashtaka ya kutumia madaraka yake vibaya, atazikwa kijeshi.