Misri kuweka kumbukumbu majeneza yenye zaidi ya miaka 2500

0
443

Wataalam wa mambo ya kale kutoka Misri wametangaza kupatikana kwa majeneza 59 ya mbao yaliyohifadhiwa vizuri na kufungwa ambayo yalizikwa zaidi ya miaka 2,500 iliyopita.

Kabla ya mkutano na vyombo vya habari vilivyokusanyika Jumamosi, timu ya wanasayansi walifunua majeneza yenye mabaki yaliyofunikwa kwa kitambaa chenye maandishi ya hieroglyphic katika rangi ang’avu.

Majeneza yote yatapelekwa kwenye jumba la kumbukumbu la “Grand Egyptian Museum” litakalofunguliwa hivi karibuni kwenye Bonde la Giza.

Ugunduzi wa majeneza hayo ulitangazwa tangu kuzuka kwa COVID-19 huko Misri, ambayo ilisababisha kufungwa kwa majumba ya kumbukumbu na maeneo ya akiolojia kwa miezi mitatu tangu mwishoni mwa Machi.

Sanamu kadhaa zilipatikana pia katika eneo hilo pamoja na sanamu ya shaba inayoonyesha Nefertem, Mungu wa zamani wa maua ya lotus.

Uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa majeneza “sarcophagi” yanawezekana yalikuwa ya makuhani, mkuu wa serikali na watu mashuhuri katika jamii ya zamani ya Misri.