Wakili wa Kenya Miguna Miguna, amedai kuwa kampuni ya ndenge ya Lufthansa ya Ujerumani imemzuia kusafiri kwa ndege kuelekea nchini Kenya mapema hii leo.
Miguna amesema kwamba kampuni hiyo imemzuia hadi pale itakapopata idhini kutoka serikali ya kenya kuwa kiongozi huyo anaweza kuondoka jambo analodai kuwa linakiuka maagizo ya mahakama.
Ndege ya shirika la Lufthansa aliyokuwa asafiri nayo kuelekea Kenya ilipangwa kuondoka Ujerumani leo saa tano asubuhi na kuwasili Nairobi saa tatu usiku.
Hatua hiyo ya miguna kurejea nchini kenya inakuja kufuatia mahakama ya juu ya Kenya kutoa agizo la kuitaka serikali ya nchi hiyo kutomzuia wakili huyo kurejea nchini humo.