Miaka 30 mauaji ya Kimbari

0
321

Leo ni maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 30 ya Mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani nchini Rwanda. Kwa maadhimisho haya Wanyarwanda wanampa kongole askari wa RPA/RPF, wakiongozwa na Paul Kagame ambaye ni Rais wa sasa wa Rwanda kwa kufanikiwa kusimamisha mauaji hayo ya kimbari. Kwa Wanyarwanda hii ni miaka 30 ya kuponyesha madonda ya mauaji, uvumilivu, umoja na kujenga nchi yao. Wenyewe wanasema Kwibuka 30 (Twiyubaka).