Meli kubwa yatia nanga Tanga

0
245

Bandari ya Tanga imepokea meli kubwa yenye shehena ya tani zaidi ya 6,600 iliotoka Urusi kwenda Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kupitia bandari hiyo.

Meneja wa bandari mkoa wa Tanga, Masoud Mrisha amesema ujio wa meli hiyo umetokana na maboresho yaliofanywa na serikali ya uchimbaji wa kina na ujenzi wa gati.

Zaidi ya shilingi bilioni 400 zimetumika kufanya maboresho kwenye bandari hiyo, ambapo mkandarasi anatarajia kukabidhi mradi huo Aprili 4 mwaka huu.