Marubani Kenya Airways warejea kazini

0
196

Marubani wa Shirika la Ndege la Kenya (Kenya Airways) wamerejea kazini baada ya mgomo uliodumu kwa siku kadhaa.

Marubani hao ambao wako chini ya Muungano wa Marubani wa Kenya (KALPA) wamerejea kazini kufuatia amri ya mahakama ya kazi ya nchi hiyo.

Katika uamuazi wake, mahakama hiyo iliagiza marubaji hao warejee kazi bila masharti yoyote na kwamba madai yao mengine yaendelee kushughulikiwa na mamlaka husika.

Marubani hao wa Shirika la Ndege la Kenya waligoma wakishinikiza kuboreshewa mazingira ya kazi pamoja na kulipwa stahili zao mbalimbali.

Mgomo huo umesababisha kufutwa kwa safari nyingi za ndege za shirika hilo na hivyo kuathiri maelfu ya wasafiri waliouwa wasafiri kwa kutumia ndege za shirika hilo.