Marekani yapiga marufuku wasafiri kutoka Brazil

0
378

Rais Donald Trump wa Marekani amepiga marufuku wasafiri kutoka nchini Brazil kuingia nchini humo, lengo likiwa ni kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya corona kutoka nje.

Marufuku hiyo inawahusu abiria wote waliokuwa nchini Brazil katika muda wa wiki mbili zilizopita.

Hata hivyo habari zaidi kutoka nchini Marekani zinaeleza kuwa, marufuku hiyo dhidi ya wasafiri kutoka Brazil itakayoanza kutekelezwa siku ya Alhamisi haiwahusu raia wa Marekani na wale wenye vibali vya kudumu vya kuishi nchini humo

Tayari Marekani imekwishazuia safari za ndege kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya, Uingereza na China.

Marekani inaongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona ikifuatiwa na Brazil na Russia.

Brazil ina zaidi ya watu laki tatu na arobaini elfu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya corona na tayari watu takribani elfu 22 wamefariki dunia baada ya kuugua corona.