Marekani yaliwekea vikwazo Jeshi la China

0
2322

Marekani imeliwekea vikwazo jeshi la China kufuatia hatua yake ya kununua ndege za kijeshi pamoja na makombora ya kurushwa kutoka ardhini kutoka nchini Russia.

Hivi karibani jeshi hilo la China lilinunua ndege kumi aina ya Sukhoi Su-35 na mtambo wa Kuzuia mashambulizi ya anga aina ya S-400 kutoka Russia.

Uhusiano wa Marekani na Russia ulianza kudorora ghafla mwaka 2014 baada ya Russia kulimega eneo la Crimea kutoka Ukraine.

Madai ya Russia kuingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 na Russia kuhusika kijeshi nchini Syria kumezidi kuzorotesha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Hata hivyo habari kutoka nchini Russia zinasema kuwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Jeshi la China havitakuwa na madhara yoyote kwa mauzo ya ndege na makombora kutoka nchini humo.

China, India na Vietnam ndio wanunuzi wakuu wa silaha za Russia.