Marekani kusitisha safari zake mashariki ya kati.

0
303

Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kuwa si busara kwa ndege za nchi hiyo kufanya safari zake katika nchi za Iran, Iraq, na Lebanon, kwani chochote kinaweza kutokea.

Nchi hiyo ambayo awali ilitangaza kuwa setelite zake ziko katika anga za juu za nchi hizo imesema, safari za anga za mashirika yake ya ndege kwenye nchi hizo ni hatari kwa vile huenda kwa makosa zikashambuliwa, zikifikiriwa kuwa ni ndege za adui.

Nchini Lebanon wapiganaji wa kikundi cha Hizboullah cha nchini humo walitangaza kuwa askari wa jeshi la Marekani na vituo vyake vya kijeshi huko mashariki vitashambuliwa ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi.

Wapiganaji wa kikundi cha Hizboullah walikasirishwa na hatua ya serikali ya Marekani kumuua kwa kombora, kamanda wa kikosi cha Quds, Qassim Soleiman cha nchini Iran, alipokuwa nchini Iraq, hali iliyosababisha hali ya taharuki nchini humo.