Malkia Elizabeth II wa Uingereza amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96.
Taarifa kutoka Kasri ya Buckingham imethibitisha kifo cha Malkia Elizabeth II ambaye amekuwa malkia kwa takribani miaka 70.
Mapema hii leo kumekuwa na taarifa kuwa hali ya afya ya Malkia imezorota, ambapo pia wanafamilia wa karibu walikusanyika kwenye Kasri la Balmoral nchini Scotland.
Habari zaidi zilieleza kuwa madaktari wa Malkia Elizabeth walishauti awe chini ya uangalizi wa karibu kutokana na hali yake ya kiafya ilivyo.