Malkia Elizabeth atimiza miaka 70 ya utawala

0
178

Wananchi wa Uingereza pamoja na makoloni ya Taifa hilo wameanza sherehe za siku nne kuadhimisha miaka sabini tangu Malkia Elizabeth wa nchi hiyo alipotangazwa kuwa malkia.
 
Hivi sasa Malkia Elizabeth ana umri wa miaka 96 na katika historia ya dunia hakuna mtawala aliyedumu muda mrefu kuliko yeye.
 
Alizaliwa mjini London tarehe 21 Aprili mwaka 1926 akiwa ni mtoto wa kwanza wa mfalme George VI wa Uingereza na Elizabeth Bowes-Lyon na kupewa jina la Elizabeth Alexandra Mary Windsor.
 
Alitangazwa kuwa malkia wa Uingereza tarehe 6 mwezi Februari mwaka 1952 mara baada ya kifo cha baba yake George VI.
 
Sherehe hizo za siku nne kuadhimisha miaka sabini tangu Malkia Elizabeth wa Uingereza alipotangazwa kuwa malkia zinaambatana na matukio mbalimbali yakiwemo maonesha ya ndege za kijeshi za nchi hiyo.