Malawi imefikia uamuzi wa kufungua ubalozi nchini Israeli katika Mji wa Yerusalemu na kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuwa na ubalozi mjini humo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Eisenower Mkaka amesema jambo hili litasaidia kukuza uhusiano kati ya Malawi na Israeli.
Jerusalem ni mji ambao umekuwa ukitumiwa na Wapalestina pamoja na Waisraeli kama mji mkuu wa nchi zao. Marekani ilikuwa nchi ya kwanza kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Yerusalemu baada ya kuutambua kama Mji Mkuu wa Yerusalemu.
Malawi inakuwa nchi ya tatu duniani kufungua ubalozi wake Yerusalemu baada ya Marekani na Guatemala.
Ubalozi huo wa Malawi nchini Israeli unatarajiwa kufunguliwa rasmi mwaka 2021.