Majaliwa afika yanapotengenezwa mabehewa ya SGR

0
266

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa mabehewa mapya kwa ajili Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania, yanayotengezwa
na kampuni ya Sung Shin Rolling Stock ya Korea Kusini.

Waziri Mkuu ameyasema hayo mara baada ya kutembelea kampuni hiyo inayotengeneza mabehewa na injini za treni iliyopo Korea Kusini.

“Kati ya mabehewa 81 ambayo Tanzania inatengeneza kutoka kwenu, tayari 36 yamekamilika na yameshapelekwa nchini Tanzania na 45 yaliyobaki yanategemewa kukamilika Machi, 2023, mabehewa haya ni ya daraja la tatu na yatatoa huduma zote muhimu.” amesema Waziri Mkuu Majaliwa

Waziri Mkuu amemkaribisha Rais wa kampuni hiyo Gye Shul Park ili awekeze Tanzania kutokana na fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo mpango wa serikali wa kuendelea kuiboresha sekta ya usafiri wa reli .

Akiwa Korea Kusini, Waziri Mkuu Majaliwa pia ametembelea kituo cha Seamul Undong ambacho ni taswira ya maendeleo ya nchi hiyo kupitia mpango wa kuviwezesha vijiji.

Kituo hicho kinatekeleza mpango kama huo nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro (Pangawe) na Zanzibar.