Watu kadhaa wanahofiwa kufa baada ya mafuriko kuyakumba maeneo kadhaa ya jimbo la Darfur Magharibi mwa Sudan, ambako mvua kubwa zinaendelea kunyesha nchini humo.
Juhudi za uokoaji zinaendelea, huku watu wanaoishi katika maeneo ya mabondeni wakitakiwa kuhamia katika maeneo yenye usalama.
Habari Zaidi kutoka Sudan zinaeleza kuwa, nyumba pamoja na mifugo katika jimbo hilo la Darfur vimesombwa na maji katika mafuriko hayo.
Wataalam wa hali ya hewa nchini Sudan wamesema, mvua kubwa zitaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.