Madhara ya Kimbunga Kenneth nchini Msumbiji

0
377

Umoja wa Mataifa umesema kuwa, hali nchini Msumbiji ni mbaya hasa eneo la Kaskazini la nchi hiyo, baada ya kukumbwa na Kimbunga Kenneth.

Kimbunga Kenneth kiliipiga Msumbiji Alhamisi iliyopita, kikiwa na upepo mkali wenye kasi Kilomita 220 kwa saa, na kusababisha mvua kubwa iliyoleta mafuriko.

Habari zaidi kutoka nchini Msumiji zinasema kuwa takribani wakazi Laki Saba nchini humo hawana mahali pa kuishi, baada ya makazi yao kusombwa na mafuriko, mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, hali ni mbaya zaidi katika miji ya Macomia, Quissanga na katika Kisiwa cha Ibo.