Macron aongoza duru ya kwanza ya uchaguzi

0
1031

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameongoza kwa kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu wa Rais uliofanyika jana nchini humo.

Katika uchaguzi huo, Macron alikua akichuana na wagombea wengine kumi na mmoja kuwania kiti hicho cha Urais.

Kulingana na matokeo hayo, katika duru ya pili Rais Macron atakutana na mgombea Marie Le Pen kutoka chama chenye siasa za mrengo wa kulia.

Duru ya Pili ya uchaguzi mkuu wa Rais nchini Ufaransa inatarajiwa kufanyika tarehe 24 mwezi huu.