Macky Sall aelekea kushinda

1
724

Waziri Mkuu wa Senegal, – Mohammed Dionne amesema kuwa Rais Macky Sall  wa nchi hiyo anaelekea kushinda kiti cha urais kwa muhula wa pili kufuatia uchaguzi uliofanyika Jumapili Februari 24.

Dionne amewaambia waandishi wa habari kuwa matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Sall amepata asilimia 57 ya kura zote zilizopigwa na kwamba matokeo rasmi ya uchaguzi huo yatatolewa siku chache zijazo.

Wapinzani wa karibu wa Rais Sall katika kinyang`anyiro hicho ambao ni Idrissa Seck and Ousmane Sonko wamesema kuwa hawaamini kama kiongozi huyo ameshinda kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa na hivyo lazima kuwepo na duru ya pili ya uchaguzi.

Duru ya Pili ya uchaguzi wa Rais nchini Senegal imepangwa kufanyika Machi 24 mwaka huu ikiwa hakutakua na mgombea aliyeshinda kwa zaidi ya asilimia 50.

Comments are closed.