Mabomu yaua watu 100 Mogadishu

0
203

Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amesema idadi ya watu waliouawa katika milipuko miwili ya mabomu iliyotokea katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu, ni zaidi ya mia moja.

Amesema miongoni mwa watu waliouawa katika milipuko hiyo ni wanawake na watoto, na kuyaita mauaji hayo kuwa ni ya kikatili.

Rais Hassan Sheikh Mohamud ameiomba Jumuiya ya Kimataifa kutoa msaada wa matibabu kwa majeruhi takribani 300 waliopata majeraha makubwa kufuatia milipuko hiyo.

Rais huyo wa Somalia amewashutumu wanamgambo wa Al-Shabab wa nchini humo kwa kuhusika na milipuko hiyo ya mabomu iliyolenga jengo la wizara ya Elimu la nchi hiyo.