Maandamano Hong Kong Yahatarisha Amani

0
235

Mtendaji mkuu wa Hong Kong Carrie Lam amesema kuwa maandamano dhidi ya serikali huko Hong Kong yanazidi kuhatarisha hali ya amani na maendeleo ya uchumi wa Hong Kong.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, mtendaji huyo wa Hong Kong amewataka waandamanaji hao kutafakari kwa kina juu  ya hatima ya maandamano hayo aliyosema yanaipeleka Hong Kong katika shimo kubwa la giza.

Hata hivyo waandamanaji hao wameendelea kukusanyika katika uwanja wa ndege ikiwa ni sehemu ya waandamanaji hao kupaza sauti juu ya madai yao dhidi ya serikali ya Hong Kong ambapo huduma za usafiri kiwanjani hapo zimeanza hii leo baada ya kusitishwa hapo jana kufuatia waandamanaji kuzingira sehemu ya ndani ya uwanja huo.