China imetangaza kupungua kwa kiwango cha maambukizi mapya ya virusi vya corona kwa siku tatu mfululizo.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya ya China imeeleza kuwa, kwa siku ya leo wagonjwa wapya 2,009 wamepokelewa katika vituo mbalimbali huku vifo 142 vikiripotiwa, idadi ambayo imesema ni ndogo ikilinganishwa na ya siku kadhaa zilizopita.
Mpaka sasa, zaidi ya watu elfu 68 wamethibitika kuugua homa ya virusi vya corona nchini China, na waliofariki dunia ni 1,665.
Wagonjwa wengine mia tano wamegundulika katika nchi takribani Thelathini, ambapo wanne wamefariki dunia huko Hong Kong, Ufaransa, Ufilipino na Japan.