Habari zinasema watu 2700 wameripotiwa kufa kwa siku moja ya Jumatano pekee ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi cha vifo kuwahi kuripotiwa tangu kuanza kwa ugonjwa huo nchini Marekani.
Watu laki moja wamefikishwa Hospitali kwa ugonjwa huo katika kipindi cha siku moja huku wengine laki mbili wakiripotiwa kuwa na maambukizi mapya nchini Marekani.
Wakazi wa jiji la Los Angeles wametakiwa kukaa ndani kutokana na ongezeko la ugonjwa huo huku wakitakiwa kuchukua hatua zaidi za tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.
Nchini Brazil katika kipindi cha saa 24 zilizopita zaidi ya watu elfu hamsini wameripotiwa kufikishwa Hospitali wakiwa na ugonjwa wa Covid 19.
Waziri wa Afya nchini Marekani, Alex Azar amesema chanjo ya covid 19 inatarajiwa kuanza kutumika nchini humo wiki ijayo