Libya yajitoa kwenye mazungumzo

0
395

Serikali ya mpito nchini Libya inayotambulika kimataifa imetangaza kujitoa katika mazungumzo ya amani ya nchi hiyo yanaofanyika nchini Ujerumani, baada ya mbabe wa kivita nchini humo Jenerali Khalifa Hafter kufanya mashambulio mapya.

Majeshi ya Jenerali Hafter yamefanya mashambulio katika uwanja wa ndege wa mjini Tripoli unaotegemewa kwa safari za anga, wakati mazungumzo hayo ya amani yakiendelea.

Serikali ya Libya imesema kuwa, mashambulio hayo yaliyofanywa na majeshi ya Jenerali Hafter yanaashiria kuwa mbabe huyo wa kivita hayuko tayari kwa amani.

Majeshi ya Hafter yalianza mashambulio dhidi ya Serikali hiyo ya Libya baada ya kutangaza kuwa yanakwenda mjini Tripoli kutwaa madaraka, na kuwatokomeza waasi waliokuwa wamesalia katika eneo hilo.