Mayanda Nzau, maarufu “Mutu Ekeko” (Mtu Sanamu), amejizolea umaarufu mkubwa katika Jiji la Kinshasa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kutoka na uwezo wake wa kujigeuza kuwa kama sanamu.
Kijana huyu mwenye umri wa miaka 31 baada ya kujisaidia haja kubwa na ndogo asubuhi, anaweza kusimama kwa muda wa saa kumi bila kujitikisa na kuwaacha watu wakibishana kama ni mtu au la.
Kipaji chake hicho alichoanza kukiibua akiwa chuo kikuu kwa kuigiza sanamu lililokuwa getini chuoni hapo, kimempa ajira mbali na kualikwa kwenye matukio mbalimbali zikiwemo dhifa za kitaifa nchini mwake.
Mayanda, ameajiriwa na Idara ya Serikali ya Makumbusho na kwa sasa yeye ni moja ya vivutio muhimu!