Kumbunga chawaacha maelfu bila huduma Marekani

0
226

Habari kutoka nchini Marekani zinaeleza kuwa hasara iliyopatikana baada ya nchi hiyo kukumbwa na kimbunga IDA inaweza kuwa sawa da dola za Marekani bilioni 95.

Kimbunga IDA kimesababisha maafa na uharibifu wa mali na miundombinu baada ya kuikumba nchi ya Marekani, huku katika baadhi ya maeneo, maji yaliyotokana na kimbunga hicho yakiingia katika nyumba za watu na baadhi ya maeneo kwa kushitukiza.

Watu walioathiriwa zaidi na mafuriko yaliyotokana na kimbunga IDA ni pamoja na wale wasiokuwa na makazi maalum, watoto yatima na wahamiaji, ambapo maji hayo yalivamia makazi yao.

Meya wa mji wa Washington, Kathy Hochul amesema serikali ya mji wake itakalazimika kupitisha sera mpya za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na mafuriko katika mji wake.

Amesema hii ni mara ya kwanza kwa mji wa Washington kushuhudia mafuriko makubwa na ya kushtukiza kama hayo.

Maeneo mengi ya mji huo na katika sehemu zingine nchini Marekani hayana huduma ya umeme, baada ya nguzo za umeme kuathiriwa na kimbunga hicho.

Rais Joe Biden wa Marekani anatarajiwa kutembelea maeneo ya New York na New Jersey, yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko ya kimbunga IDA.