Kindiki rasmi amrithi Gachagua Naibu Rais Kenya

0
252

Profesa Kithure Kindiki ameapishwa kushika rasmi wadhifa wa Naibu Rais wa Kenya.

Hafla ya kumuapisha Profesa Kindiki imefanyika leo Novemba Mosi, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (K.I.C.C.) Jijini Nairobi na kuhudhuriwa na viongozi, wananchi na wageni mbalimbali.