Kimbunga Tauktae chasababisha vifo

0
170

Zaidi ya watu Ishirini wamefariki dunia nchini India,  baada kimbunga kikali kinachojulikana kama Tauktae kulikumba eneo la Magharibi la nchi hiyo.

Habari zaidi kutoka nchini India zinaeleza kuwa, watu wengine 96 hawajulikani walipo kufuatia kimbunga hicho kilichoambatana na mvua kubwa pamoja na upepo mkali.

Watu hao ambao hawajulikani walipo ni miongoni mwa watu 270 waliokuwemo ndani ya boti ya uokoaji ambayo imezama kwenye maji wakati wa zoezi la uokoaji likiendelea.

Kimbunga hicho Tauktae kilikuwa na kasi ya kilomita 185 kwa saa,  na mpaka sasa kimesababisha maelfu ya watu katika eneo hilo la Magharibi mwa India kukosa huduma muhimu ikiwa ni pamoja na nishati ya umeme na mawasiliano ya barabara.

India imekumbwa na kimbunga hicho kikali katika kipindi hiki ambacho pia inakabiliwa na maambukizi makubwa ya virusi vya corona.