Ofisi ya kitaifa ya kupambana na majanga nchini Madagascar imesema leo Machi 28, 2024, kimbunga Gamane kilichokuwa kimekadiriwa kukivuka kisiwa hicho cha Madagascar kilicho katika Bahari ya Hindi, kilibadilisha mwelekeo na kupiga katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.Mamlaka zimesema watu sita wamezama majini na wengine watano wamefariki kutokana na kuangukiwa na miti au nyumba, huku watu elfu saba wakiathirika na kimbunga hicho.Chanzo: DW