Bendera ya Umoja wa Mataifa (UN) itapepea nusu mlingoti katika Makao Makuu yake yaliyopo New York Marekani katika siku ya Mazishi ya aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli.
Hatua hiyo ya UN ni kuungana na Watanzania na nchi wanachama kuomboleza kifo cha Mwana-Afrika huyo.
Rais Magufuli alifariki Machi 17, 2021 kwa maradhi ya moyo na anatarajiwa kuzikwa Machi 26, mwaka huu wilayani Chato, mkoani Geita.