Kesi ya Al Bashir yaanza kusikilizwa

0
188

Serikali ya Sudan imeanza kusikiliza kesi ya madai inayomkabili aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Omar Al Bashir, ambaye aliondolewa madarakani na kisha jeshi kutwaa madaraka.

Al Bashir anatuhumiwa kutumia madaraka yake vibaya  pamoja na kuhodhi mali ambazo ni za serikali.

Tuhuma nyingine zinazomkabili Rais huyo wa zamani wa Sudan ni kuhusika na vitendo vingine vya uhalifu, ikiwemo ukatili dhidi ya raia.