Kenya na Marekani zimekubaliana kuanza mazungumzo yenye lengo la kufanikisha makubaliano ya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.
Makubaliano hayo yamefikiwa baina ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais Donald Trump wa Marekani jijini Washington, ambapo Rais Kenyatta yuko nchini humo kwa lengo la kukutana na viongozi pamoja na wafanyabishara wa Taifa hilo.
Awali akizungumza na wafanyabiasahara mbalimbali wa nchini Marekani, Rais Kenyatta amesema kuwa mbali na Kenya kupanua wigo wa soko la bidhaa zake kwenda Marekani kwa masharti nafuu hadi ifikapo 2025, pia wana lengo la kuifanya nchi hiyo kuwa kitovu cha kampuni za Marekani zinayofanya biashara Barani Afrika.
Biashara kati ya Kenya na Marekani zinafikia dola bilioni moja za Kimarekani kwa mwaka.