Karantini China mwisho Januari 8

0
281

China imetangaza kuondoa sharti la ukaaji karantini kwa wageni wanaowasili nchini humo ambalo lilikuwa ni moja ya mikakati ya kukabiliana na maambukizi ya UVIKO19 kwa miaka mitatu mfululizo.

Pamoja na hilo China imeahidi kurejesha utaratibu wa usafiri wa raia wa China kutoka nje kama sehemu ya mpango wa jumla wa kushusha kiwango cha usimamizi wa UVIKO19 nchini humo kuanzia Januari 8, 2023.

Uamuzi huu ni hatua ya mwisho ya nchi hiyo kuelekeza kujifunza kuishi na virusi hivyo.