Ubalozi wa Tanzania
nchini Nigeria, Wenye Uwakilishi Sambamba nchini Ghana, umefanya Kongamano la
Utalii, Uwekezaji na Biashara (Tanzania-Ghana Tourism, Investment and Trade
Forum (TN-TITF), kwa lengo la kutangaza utalii na kuvutia wawekezaji kutoka
nchini Ghana kuja kuwekeza hapa nchini.
Jukwaa hilo liimefunguliwa na Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, ambapo pia
limehudhuriwa na wadau wa sekta mbalimbali ikiwemo Jumuiya za Wafanyabiashara,
Wenyeviwanda, Kilimo na Madini za Ghana, Makampuni ya Utalii, Wafanyabiashara
na Wawekezamitaji.
Aidha, Taasisi za Tanzania, hususani TTB, TIC,
ZIPA, EPZA, TanTRADE, Jumuiya za Wafanyabiashara, Wenyeviwanda, Kilimo na
Madini za Tanzania Bara na Zanzibar, zilishiriki na kuelezea kwa undani fursa,
miundo, majukumu na nafasi zake katika kukuza Biashara, Utalii na Uwekezaji
nchini Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Nigeria anbaye pia
anawakilisha nchi ya Ghana Dkt. Benson Bana, ameeleza kuwa Jukwaa hilo
linakusudia kuleta taasisi, jumuiya za wafanyabiashara, wawekezaji wa Tanzania
na Ghana kuona namna ya kushirikiana na kukuza mahusiano ya uwili baina ya nchi
hizo, ambazo uhusiano wake ulianza tangu kipindi cha waasisi wa mataifa hayo.
Kwa Upande wake Balozi Mstaafu wa Ghana nchini
Ufaransa, Genevieve Delali Tsegah, amepongeza hatua hiyo na kusema kuwa
itakwenda kufungua milango ya utalii na uwekezaji nchini Tanzania kutokana na
kazi kubwa inayofanywa na viongozi wake