Joe Biden kuwania Uraisi Marekani

0
207

Joe Biden amechaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa kitaifa wa Chama cha Democratic nchini Marekani kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu.

Marais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton na Jimmy Carter, wameunga mkono kuchaguliwa kwa Biden na kusema ni kuwa mtu mwenye uzoefu na uadilifu.

Hii ni mara ya tatu kwa Biden kuingia kwenye kinyang’anyiro cha urais wa Marekani.