Kampuni ya dawa ya Janssen ambayo ni kampuni tanzu ya Johnson and Johson ya nchini Marekani, imesitisha awamu ya tatu ya majaribio ya chanjo dhidi ya Ukimwi.
Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, kampuni hiyo imesema chanjo hiyo imeonekana kutokuwa na ufanisi wa kuzuia maambukizi ya VVU ikiwa imeshafika hatua za juu za majaribio.
Chanjo hiyo dhidi ya Ukimwi iliyofamyiwa majaribio na kampuni ya dawa ya Janssen, imewekwa katika orodha ya chanjo ambazo zimejaribiwa lakini hazikuweza kutoa mwitikio chanya wa kinga ya kuzuia maambukizi.
Ingawa teknolojia ya kisasa imefaulu kutengeneza chanjo dhidi ya virusi mbalimbali, imekuwa vigumu kwa kirusi cha Ukimwi kwa kuwa kinasifa ya kukwepa mfumo wa kinga kutokana na tabia yake ya kubadilika mara lwa mara na kwa wepesi.