Israel yatishia kushambulia Rafah

0
208

Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Israel Kuhusu Vita, Benny Gantz ameonya kwamba kama Hamas haitawaachilia huru mateka wote wanaoshikiliwa Gaza hadi kufikia Machi 10, 2024, Israel itaanza kuupiga mabomu mji wa Rafah.

Rafah ni mji wa kusini mwa Gaza ambao sasa una msongamano mkubwa wa watu kutokana na Wapalestina kukimbilia huko kujihifadhi dhidi ya mashambulizi ya Israel yaliyoua takribani watu 29,000.

Hata hivyo, nchi mbalimbali duniani zimekuwa zikipinga vikali mpango wa Israel kutaka kushambulia Rafah.