Israel yaangusha ndege 300 za Iran

0
1914

Marekani imewapongeza askari wake ambao wametoa msaada kwa vikosi vya Israel kuangusha takribani ndege zote 300 zisizo na rubani na makombora yaliyorushwa na Iran leo Aprili 14, 2024.

Pongezi hizo zimetolewa na Rais Joe Biden wa Marekani baada ya mazungumzo yake aliyodai kuyafanya kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Awali Israel ilisema Iran imetuma ndege kadhaa sizizo na rubani na makombora kuelekea upande wake, ikiwa ni mara ya kwanza nchi hiyo kuishambulia Israel moja kwa moja kutoka katika ardhi yake.

Hivi karibuni Iran ilionya kuwa Israel itaadhibiwa kufuatia hatua yake ya kuushambulia ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria Aprili Mosi mwaka huu ambapo maafisa saba wa Iran waliuawa.

Hata hivyo Israel haijathibitisha au kukanusha ikiwa ilihusika na shambulio hilo.