Iran yaishutumu Marekani ajali ya ndege ya Ukraine

0
432

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Javad Zarif amesema kuanguka kwa ndege ya Ukraine mjini Tehran wiki iliyopita ni matokeo ya mambo mabaya ambayo nchi ya Marekani imekuwa ikifanya dhidi ya nchi yake.

Zarif amesema hivi sasa nchi hiyo inashindwa kudhibiti maandamano hasa ya wanafunzi wanaondamana kupinga hatua ya majeshi ya Iran kutungua kwa bahati mbaya ndege ya abiria ya Ukraine na kusababisha vifo vya abiria wote 176 waliokuwa ndani yake.

Baadhi ya watu waliokufa katika ajali hiyo walikuwa wanafunzi wa vyuo vikuu, na Marekani ilitangaza kuwa inaunga mkono maandamano yao, na serikali ya Iran haina sababu ya kuwazuia.