Iran kukishikilia kisanduku cheusi cha Ndege ya Ukraine

0
306

Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Iran imesema kuwa haitoikabidhi Kampuni ya Boeing kisanduku cheusi (black box) cha ndege ya Ukraine iliyoanguka leo jijini Tehran na kupelekea vifo vya watu 176.

Ali Abedzadeh, mkuu wa mamlaka hiyo amesema uamuzi huo umechuliwa kutokana na kuwapo mkanganyiko wa wapi kisanduku hicho kipelekwe kati ya Marekani, ilipo kampuni hiyo, au Ukraine ambayo ndiyo mmiliki wa ndege iliyoanguka.

Kisanduku hicho hukusanya taarifa za mwenendo wa ndege zinazotumika katika kuchunguza ajali za ndege na kuweza kubaini chanzo cha ajali au matukio mengine yasiyo ya kawaida.

Ndege hiyo ya la Ukraine imeangua leo alfajiri muda mfupi baada ya kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini, Tehran na kuuawa watu wote.

Waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na raia 82 wa Iran, 63 wa Canada, 11 wa Ukraine. Wengine ni raia 10 wa Sweden, 4 wa Afghanistan, 3 wa Uingereza na 3 kutoka Ujerumani.