IMF yatoa neno vita vya Russia na Ukraine

0
1478

Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) limeonya kwamba kupanda ghafla kwa bei za bidhaa kutokana na athari za vita vya Russia na Ukraine, kunahatarisha amani na ustawi wa mataifa mengine duniani.

Maafisa wa shirika hilo wamesema athari za vita hivyo zinazilazimisha nchi masikini kukopa zaidi, huku bado zikiwa na mzigo wa madeni kutokana na athari za janga la UVIKO – 19.

Wamesema karibia asilimia 60 ya mataifa yenye kipato cha chini duniani yako katika mgandamizo wa madeni, hatua ambayo imekuwa ikisababisha manung’uniko kutoka kwa Wananchi ambao hulazimika hata kuandamana kushinikiza Viongozi walioko madarakani wajiuzulu.