Huduma ya umeme kuimarika Desemba

0
116

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewahakikishia wananchi kuwa huduma ya umeme itaimarika kuanzia mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja kutoka TANESCO Martin Mwambene amesema, huduma hiyo itaimarika baada ya mitambo ya kuzalisha umeme ya Kidatu inayozalisha megawati 50 za umeme na ile ya Ubungo III inayozaliwa megawati 20 za umeme kutengemaa siku chache zijazo.

Amesema mtambo wa Kinyerezi I utakaozalisha megawati 80 za umeme, nao ufungaji wake utakuwa umekamilika hadi kitakapofika kipindi hicho cha mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.

Kaimu Mkurugenzi huyo wa Huduma kwa Wateja kutoka TANESCO ameongeza kuwa ukame ni miongoni mwa sababu za kukosekana kwa huduma ya umeme ya uhakika, lakini mwezi huo wa Desemba upatikanaji wa huduma hiyo utaimarika maradufu.

Naye Mhandisi Mkazi wa mradi wa Kufua Umeme wa maji wa Bwawa la Julius Nyerere Lutengano Mwandambo amesema, utkelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 77 na mpaka sasa takribani shilingi trilioni 4.4 zimetumika.

Hadi kukamilika kwake mradi huo utakuwa umegharimu shilingi trilioni 6.5