Serikali ya Nigeria imetangaza hali ya tahadhari katika eneo la kati la nchi hiyo, baada ya kutokea mauaji makubwa yaliyosababishwa na shambulio la kigaidi.
Katika tukio hilo, watu wenye silaha waliwashambulia kwa bunduki na kuwaua watu 46, mauaji yanayoonekana kuwa na mwelekeo wa chuki za kidini, kwani walengwa walikuwa ni waumini wa dini ya Kikristo.
Tayari polisi nchini Nigeria wamewakamata watu 10 wanaotuhumiwa kuhusika na shambulio hilo lililotokea hapo jana.