Taarifa iliyotolewa na kituo cha Televisheni cha Serikali ya Iran zimesema hakuna dalili za watu kuwa hai kufuatia kuanguka kwa helikopta iliyombeba Rais wa nchi hiyo Ebrahim Raisi pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo IHossein Amir-Abdollahian.
Awali ilielezwa kuwepo kwa hali mbaya ya hewa ukiwepo ukungu mwingi katika eneo ilipotokea ajali hiyo, hali iliyoifanya helkopta hiyo kupata wakati mgumu wakati wa kutua wakati Rais huyo na ujumbe wake wakielekea
katika mji wa Tabriz uliopo Kaskazini Magharibi mwa Iran.
Shirika la Mwezi Mwekundu limesema tayari timu ya waokoaji imepata eneo ilipoanguka helikopta hiyo huku likisisitiza kuwa hali sio nzuri bila kueleza zaidi.
Helikopta hiyo ni miongoni mwa helikopta tatu zilzokuwa katika msafara huo, ambapo mbili inaelezwa zilitua salama.
Kabla ya ajali hiyo kutokea, Rais huyo wa Iran alishiriki katika ufunguzi wa mabwawa mawili karibu na mpaka wa Iran na Azerbaijan.
Raisi alichaguliwa kuwa Rais wa Iran mwaka 2021.