Hakainde Hichilema rasmi Rais wa Zambia

0
244

Rais Hakainde Hichilema  wa Zambia amewataka Raia wa Taifa hilo kutembea kifua mbele wakitambua kuwa nchi hiyo ni mali yao na si ya kiongozi yeyote.

Akihutubia Wananchi katika uwanja wa Taifa wa Mashujaa jijini Lusaka mara baada ya kuapishwa, Rais Hichilema amewataka Wazambia wote hasa vijana kufanya kazi kwa bidii ili kuendelea kuliletea maendeleo Taifa hilo.

Ameahidi kushirikiana na Viongozi na Wananchi wote wa Zambia ili kuhakikisha yale yote aliyoyaahidi wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu uliopita yanatekelezwa.

Rais Hichilema kutoka chama cha United Party for National Development (UPND),  ameapishwa kuwa Rais wa Saba wa Zambia baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika tarehe 12 mwezi huu

Katika kinyang’anyiro cha Urais, Hichilema  alimshinda mpinzani wake Edgar Lungu aliyekuwa akitetea kiti hicho.