Ghana wanapiga kura kumchagua Rais na Wabunge 

0
211

Wananchi wa Ghana wanaendelea kupiga kura kumchagua Rais wa nchi hiyo na Wabunge.

Rais Nana Akufo Addo anayewania kiti cha Urais kwa kipindi cha pili,  anakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa rais wa zamani wa Ghana, -John Mahama.

Habari zaidi kutoka nchini Ghana zinaeleza kuwa watu walianza kujipanga kwenye mistari kwa ajili ya kusubiri kupiga kura toka usiku wa kuamkia hii leo.

Huo ni uchaguzi wa nane wa Ghana tangu kurejea kwa mfumo wa vyama vingi nchini humo mwaka 1992.

Zaidi ya watu milioni 17 wamejiandikisha kupiga kura nchini Ghana.

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa saa moja asubuhi na vinatarajiwa kufungwa saa 11 jioni.