George Weah kuwania kipindi cha pili cha Urais

0
247

Rais George Weah wa Liberia ametangaza kuwania kiti hicho kwa kipindi cha pili, katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Akilihutubia Taifa ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kuanza kwa mwaka huu, Mwanasoka huyo wa zamani amewataka raia wa Liberia kumpa nafasi ya kuongoza kwa kipindi cha pili ambacho atahudumu kwa miaka sita.

Utawala wa Rais Weah umekuwa ukishutumiwa kwa kutoshughulikia migogoro ya kiuchumi ambayo imekuwa ikijitokeza nchini humo.

George Weah mwenye umri wa miaka 56, aliingia madarakani mwaka 2018.