Gavana wa Nairobi Mike Sonko apigwa chini

0
158

Bunge la Seneti nchini Kenya limepiga kura kumuondoa gavana wa Nairobi Mike Mubuvi Sonko katika uongozi baada ya kuongoza kwa miaka mitatu.

Sonko anatuhumiwa kwa ukiukaji wa katiba, matumizi mabaya ya madaraka, utovu wa nidhamu, na uhalifu chini ya sheria.

Maseneta 27 walipiga kura kuunga mkono kuondolewa kwa Sonko baada ya taarifa iliyowasilishwa na Bunge la Kaunti ya Nairobi ambalo lilipiga kura ya kutokuwa na imani naye tangu Desemba 3.

Kuondolewa madarakani kwa Sonko kumetoa nafasi kwa Spika wa Bunge la Kaunti ya Nairobi Ben Mutura kushika nafasi yake hadi uchaguzi wa gavana na naibu wake utakapofanyika tena katika kipindi cha siku 60 zijazo.